Habari ndugu yangu! karibu dawaasili.co.tz
Fibroids au uvimbe ndani ya kizazi cha mwanamke, ni uvimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha, unaoota na kukua kwenye nyumba ya uzazi (uterus). Majina mengine ya uvimbe huu ni uterine fibroids, myomas, au fibromyomas. Fibroids ni aina ya uvimbe unaoonekana kwa wingi zaidi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke.
AINA ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI
- INTRAMURAL FIBROID
Hii ni aina maarufu Zaidi na zinawatokea zaid wanawake. Aina hii ya fibroid hukua na kumea
kwenye misuli ya ukuta wa uterus na kusababisha kupanuka au kuvutika kwa kizazi na
kusababisha dalili kama hedhi ya muda mrefu inayoambatana na nyonga. - SUBSEROSAL FIBROID
Aina hii ya fibroidshukua nje ya ukuta wa mfuko wa mimba, wakati mwingine kuelekea kwenye
kibofu cha mkojo. Aina hii huweza kusababisha maumivu ya mgongo kutokana na kwamba
uvimbe huu unasukuma nerve za spinal na kusababisha presha kubwa kwenye eneo la chini ya
mgongo. - SUBMUCOSAL FIBROID
Aina hii ya fibroid hukua karibu na ukuta wa uterus na inaweza kusababisha bleed ya muda
mrefu na shida kenye kushika ujauzito - CEVICAL FIBROID
Hizi hukua kwenye tishu za mlango wa kizazi ambao huitwa cervix. Hutokea mara chache sana
ukilinganisha na aina zingine za fibroids.
Chanzo Cha Fibroids
Sababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kukua kwa haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen.
Wanawake wanaokaribia kufikia ukomo wa kupata siku zao za mwezi wanaonekana kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids kwa sababu ya kuwa wameishi na homoni ya estrogen kwa muda mrefu zaidi.
Dalili Za Fibroids
Akina mama wengine wenye uvimbe wa fibroids huwa hawaoni dalili zo zote zile (wengi hawajui kama wana fibroids) au kuona dalili kidogo na kwa wengine dalili hizi hujitokeza sana na kuwasumbua hadi kufikia kutafuta tiba. Baadhi ya dalili za fibroids ni:
– Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku au kutokwa na damu kwa muda mrefu
– Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku au kutokwa na damu kwa muda mrefu
– Kutokawa na damu kusiko kwa kawaida katikati ya siku za mwezi
– Mauvimu ya nyonga (uvimbe kugandamiza kwenye viungo vya nyonga)
– Kupata haja ndogo mara kwa mara
– Maumivu ya mgongo
– Maumivu wakati wa tendo la ndoa
– Upungufu wa damu kwa sababu ya kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku
– Maumivu ya kichwa
– Maumivu kwenye miguu
– Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (Fibroids kubwa)
– Uzazi wa shida
– Mimba za shida
– Kutopata mimba
– Kutoka kwa mimba mara kwa mara
TIBA YA FIBROIDS KWA KUTUMIA DAWA
Tiba kubwa ya fibroids ni kwa kutumia dawa aina hii ambayo hutolewa kama syrup. Dawa hii huufanya mwili wa mwanamke upunguze utengenezaji wa estrogen hivyo kusababisha fibroids kunyauka.

